KLABU ya Chelsea imethibitisha kumsaini Kocha Antonio Conte kuwa Meneja wake mpya kwa mkataba wa miaka mitatu.
Kocha huyo anayekinoa kikosi cha timu ya taifa ya Italia 'Azzuri' atajiunga na klabu hiyo baada ya michuano ya Euro itakayofanyika nchini Ufaransa mwezi Juni.
Conte mwenye miaka 46 amesema "Nimejisiki vizuri kuchaguliwa kuwa meneja mpya wa Chelsea na pia kuwa kocha wa timu ya taifa langu hadi hapa tulipofika".
"Chelsea na soka la Uingereza linatazamwa duniani kote na mashabiki wana hisia kali ya mafanikio na ushindi uwanjani kama ilivyokuwa nchini Italia.
Conte anachukua nafasi iliyoachwa wazi Jose Mourinho ambaye alitupiwa virago mwezi Disemba baada ya kuboronga mwanzoni mwa msimu huu.
Guus Hiddink ambaye amechaguliwa kuwa kocha wa muda tangu kutimuliwa kwa Mourinho ameshasema atastaafu baada ya kumalizika kwa msimu huu.
Conte anakuwa kocha wa tano raia wa Italia kuifundisha Chelsea baada ya Gianluca Vialli, Claudio Ranieri, Carlo Ancelotti na Roberto Di Matteo.
Monday, 4 April 2016
Home
Unlabelled
ANTONIO KONTE NDIYE KOCHA MPYA WA CHELSEA
No comments:
Post a Comment