• Seynation Updates

    Saturday, 17 September 2016

    Mchungaji akatisha hotuba ya Trump ya kumpinga Clinton

    Mchungaji wa kanisa moja la watu weusi katika jimbo la Michigan, Marekani amemkatisha Donald Trump akihutubu alipoanza kumshutumu mpinzani wake Hillary Clinton.
    Mchungaji Faith Green Timmons alimkatisha BwTrump alipomshutumu mgombea huyo wa chama cha Democratic kuhusu mikataba ya kibiashara duniani.

    _91204122_hi035302611
    “Bw Trump, nilikualika hapa uje kutushukuru kwa juhudi ambazo tumefanya Flint, si kutoa hotuba ya kisiasa,” amesema pasta huyo wa kanisa la Bethel United Methodist.
    “Aha, hilo ni jambo njema,” amemjibu mgombea huyo wa chama cha Republican huku akionekana kuanza kucheza na karatasi alizokuwa nazo jukwaani.
    Bw Trump ameendelea na kuzungumzia kwa kifupi kuhusu kutatua matatizo ya maji safi Flint, lakini baadhi ya watu kwenye umati wakaanza kumzomea.
    Mwanamke mmoja amesema kwa sauti kwamba mfanyabiashara huyo tajiri alitumia njia za kibaguzi katika majumba yake.
    Mfanyabiashara huyo amejibu: “Haiwezekani, umekosea. Singeweza kufanya hivyo.”
    Mchungaji huyo ameingia tena na kuwashutumu waliokuwa wanamzomea Bw Trump na kusema: “Yeye ni mgeni katika kanisa langu na mtamheshimu”
    Bw Trump mwishowe amelazimika kukatiza ghafla hotuba yake, ambayo imedumu kwa dakika sita hivi.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI