
Msanii na mtayarishaji wa nyimbo za Bongofleva Anayetoka kwenye kundi la NavyKenzo NAHREEL, amefanikiwa kushiriki katika kuandaa wimbo maalum wa kombe la Dunia 2018 ulioimbwa na Diamond Platznumz akishirikiana na Jason Derulo.
Nahreel akiwa pamoja na Msanii Naseeb Abdul ( Diamond Platnumz) wamesaini mkataba na kukabidhiwa jukumu la kuanza kuandaa Wimbo huo wa Diamond na Jason Derulo na wengine.
Jambo hili limebainika kupitia ukurasa wa Instagram wa msanii Nahreel ambapo amepost picha 2 kwa nyakati tofauti akiwa na Diamond Platnumz na kuandika caption "Pleasure to produce the World Cup 2018 Anthem song featuring #JasonDeruloand @diamondplatnumz song called #Colors available now in all platforms #Cocacola"
Usikose habari zaidi Tufuatilie Instagram @seynation na INSTALL APP YETU BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment