• Seynation Updates

    Sunday 11 December 2016

    60 WAUAWA KANISANI NIGERIA

    Paa la kanisa katika mjini uliopo kusini mashariki mwa Nigeria, limeanguka na kusababisha vifo vya takriban watu 60. Idadi ya watu waliopoteza maisha inahofiwa kuongezeka.
    aedd7625e4e14f7aabc48ce0cb9db961_18
    Kanisa hilo la kiinjilisti la Reigners Bible Ministry kwenye mji wa Uyo katika jimbo la Ibom, lilikuwa limefurika waumini baada ya paa ambalo bado linaendelea kujengwa lilipoanguka Jumamosi hii.
    Miili ya takriban wahanga 60 imeondolewa tayari.
    Gavana Udom Emmanuel aliripotiwa kuwemo ndani ya kanisa hilo baada ya paa hilo lenye vyuma lilipoanguka japo hakujeruhiwa.
    “We have never had such a shocking incident in the history of our dear state,” Emmanuel aliandika kwenye ukurasa wa Facebook.
    Rais Muhammadu Buhari ametuma salamu za rambirambi. Shirika la habari la serikali limedai kuwa kati ya watu 50 – 200 wanaweza kuwa wamepoteza maisha.
    September 2014, watu 115 people wakiwemo 84 raia wa Afrika Kusini walipoteza maisha mjini Lagos baada ya kanisa la mchungaji maarufu TB Joshua kuanguka.
    Source: Aljazeera


    ULIKOSA HII SHOW TM manga WAKIDANCE 'INDE' BOFYA HAPA

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI