• Seynation Updates

    Thursday 5 April 2018

    BREAKING: BASI LA CITY BOY LAUA 13 TABORA 46 WAJERUHIWA.

    3.jpg

    Watu 13 wameripotiwa kupoteza maisha baada ya basi la CITY BOY kogongana uso kwa uso na Fuso, usiku wa kuamkia tarehe 5/04/2018 katika eneo la Igunga-Tabora. Basi hilo la CITY BOY lilikua likifanya safari zake kutoka Karagwe  kwenda Dar Es Salaam.

    Ajali hiyo imethibitishwa na Kamanda wa polisi wa Mkoa wa TABORA Wilbrod Mutafungwa

    Jumla ya watu 12 wamepoteza maisha , 10 eneo la tukio, 2 wakiwa wanapelekwa Hospitali ya Wilaya Igunga. Jumla ya majeruhi 46 wamefikishwa Hospitali ya Wilaya Igunga kwa matibabu, kati yao 3 ni mahututi ambapo ME 02 wamepelekwa Bugando Mwanza na KE 01 amepelekwa Nkinga usiku huu.“amesema Kamanda Mutafungwa.


    Takwimu zinaonesha kuwa basi hili la CITY BOY liliwahi kupata ajali mwaka 2016 hali  iliyopelekea kufungiwa huduma za usafirishaji kwa Mabasi hayo ya CITY BOY.

    Endelea kufuatilia Blog hii ili kujua kile kinachoendelea kuhusiana na hali za majeruhi.



    2 comments:

    1. Hey you guy huu ni upotoshaji umesema ajali hii imetokea tarehe 15 mwezi wa NNE you are not serious at all karibu kua na serious na kazi yako today is 5th April 2018

      ReplyDelete

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI