Baada ya klabu ya Yanga kuambulia kichapo cha penati nne kwa mbili katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la Mapinduzi Jumanne hii, aliyekuwa afisa habari wa klabu ya Young Africans Jerry Muro ambaye kwa sasa bado anatumikia adhabu ya kufungiwa na TFF, amewatupia dongo watani wake wa klabu ya Simba.
Mashabiki wa Klabu ya Simba amekuwa wakitaniwa mara kwa mara na mashabiki wa Yanga baada ya kufanya tukio la kuvunja viti katika uwanja wa Taifa wakati wa kicheza na watani wao wajadi Yanga.
Muro amerusha kijembe hicho kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram kwa kuandika
‘Sikilizeni nyinyi…Bora hata Simba mmeshinda, maana mlivyo watata mngeweza hata vunja Muungano’
Watani hao wa jadi wanatarajiwa kukutana tena katika mzunguko wa pili wa ligi kuu wa Tanzania bara ambayo sasa hivi imesimama kwa muda kupisha michuano ya kombe la Mapinduzi.
Ili ujue kinachoendelea Mtu wangu usiache kukaa karibu yangu kwenye FACEBOOK na INSTAGRAM @seynation ili niwe nakutumia kila kinachoonifikia.
No comments:
Post a Comment