Rapper Nay wa Mitego
Rapper huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Sijiwezi’ amedai watu wengi walikuwa na mashaka na uhalali wa mali zake ambazo amekuwa akizitaja katika vyomba vya habari.
“Mimi nipo tofauti kidogo na wasanii wengine, mimi niliamua kuwekeza kwenye baadhi ya vitu, kweye biashara za saloon, magari. Hela ambayo nilikuwa napata kwenye muziki nilikuwa naiweka kwenye biashara,” Nay alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EATV. “Watu walikuwa na mashaka lakini this time nipo free zaidi kwa sababu hata wahusika wa nchi ambao walikuwa na wasiwasi na mali zangu this time wameridhika na sasa wanaimani na mimi na wameniambia niwe mfano kwa vijana wenzangu,”
Rapper huyo alitiliwa shaka na baadhi ya watu kusuhu mali zake pamoja na utajiri wake huku wengi wakihisi huwenda rapper huyo akawa anajihusisha na biashara ya Madawa ya kulevya.
Mwezi Juni mwaka 2016 rapper huyo akiwa katika kipindi XXL cha Clouds FM alidai baada ya mwaka mmoja naweza akawa tajiri namba moja nchini Tanzania.
Ili ujue kinachoendelea Mtu wangu usiache kukaa karibu yangu kwenye FACEBOOK na INSTAGRAM @seynation ili niwe nakutumia kila kinachoonifikia.
SOURCE: BONGO 5.COM
No comments:
Post a Comment