• Seynation Updates

    Friday, 20 January 2017

    SENEGAL YATINGA ROBO FAINALI YA AFCON 2017.

    Baada ya jioni ya January 19 2017 kushuhudia mchezo wa kwanza wa Kundi B kwa January 19 katika uwanja wa Franceville ukizikutanisha timu za Tunisia dhidi ya Algeria na kushuhudia Tunisia wakipata ushindi wa goli 2-1, usiku wake ilikuw zamu ya Senegal kucheza dhidi ya  Zimbabwe katika uwanja huo.
    Mchezo wa pili wa kati ya Senegal dhidi ya Zimbabwe umedhihirisha safari ya Senegal kuingia moja kwa moja hatua ya robo fainali, hiyo ni baada ya ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Zimbabwe, magoli ambayo yalifungwa na Sadio Mane dakika ya 9 na Henri Saivet aliyefunga goli dakika ya 14 kwa mpira wa adhabu ndogo.
    Ushindi huo umeifanya Senegal kutinga hatua ya robo fainali kwa kufikisha jumla ya point sita huku wakisalia na mchezo mmoja, Senegal anaongoza Kundi B kwa kuwa na point 6, wakifuatiwa na Tunisia wenye point tatu, Algeria na Zimbabwe wakiwa nafasi ya tatu na nne kwa kuwa na point moja moja kila mmoja huku wakiwa wamepishana magoli yakufunga na kufungwa.

    Jiunge na: Seynation Media.



    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI