• Seynation Updates

    Friday 13 January 2017

    UCHAMBUZI WA MECHI YA AZAM NA SIMBA KUANZIA DAKIKA YA KWANZA HADI YA MWISHO....KOMBE LA MAPINDUZI

    MPIRA UMEKWISHAAAA
    Dk 90+3, Mkude aanaachia mkwaju hapa, lakini Manula anadaka na kuinuka kwa mbwembwe kabisa
    Dk 90+2, Stephan wa Azam FC yuko chini pale (jukwaani, mashabiki wa Simba wanaonekana kukata tamaa, wanaanza kuondoka)
    DK 90+1 Dalili zinaonyesha Simba hawana nafasi tena kutokaba ba Azam FC kuanza kupoteza muda katika dakika za mwishoni. lakini hata wachezaji wa Simba wanaonekana kukata tamaa


    DAKIKA 4 A NYONGEZA
    Dk 88, Azam FC wanaokoa hapa na kuwa konaaaaa, inachongwa na Zimbwe lakini Manula anadaka kwa ustadi kabisa hapa
    Dk 86, Kapombe analala na kuokoa mpira wa hatari langoni mwake, unakuwa wa kurusha
    Dk 85, Simba wanagongenaa vizuri hapa, Mavugo anampa Pastory lakini Azam wanaokoa hapa
    Dk 83, Manula yuko chini, hali inayoonyesha anataka kuanza kukata kasi ya mashambulizi ya Simba kwa kusingizia ugonjwa



    SUB Dk 82, Enock Atta Agyei anaingia kuchukua nafasi ya Himid aliyefunga bao pekee la mechi hii hadi sasa, kwa mkwaju matata
    Dk 78 mbele ya Banda, Bocco anajipinda na kuachia mkwaju hapa lakini gooal kick
    SUB Dk 76, Simba inamtoa Kichuya na nafasi yake inachukuliwa na Jamal Simba Mnyate
    Dk 74, Pastory anaanguka hapa, lakini mwamuzi anasema nimeona vizuri, hii ni goal kick

    Dk 74, Azam FC wanapata nafasi nyingine nzuri lakini Mudathir anapiga shuti hapa
    Dk 73 sasa, Simba wanagongeana vizuri lakini hakuna malengo hasa katika umaliziaji hukU Azam FC wengi wakiwa wamebaki nyuma ya mpira kuhakikisha wanalinda bao lao moja
    SUB Dk 70, Simba wanamtoa Muzamiru Yassin na nafasi yake inachukuliwa na Pastory Athanas
    SUB Dk 69, Azam FC wanamtoa Yahaya Mohamed na kumuingiza Mudathir Yahaya. Maana yake, sasa Azam FC wanacheza na viungo wakabaji watatu (Himid, Domayo na Mudathir) wakionyesha wamepania kulinda bao lao
    Dk 66, Mavugo yeye na kipa krosi safi ya Kichuya, anapaisha juuu



    Dk 64, wanaendelea kufanya utani katika safu ya ulinzi, Bukungu anapokonywa mpira, pasi ya Sure Boy inakwenda kwa yahya lakini Mwanjale analala chini na kuokoa huku Kotei akiwa ameugonga mpira
    Dk 63, kwa namna wanavyocheza Simba, hawawezi kuwa na matumaini ya kufunga. Wanalazimika kubadilisha aina ya mashambulizi hasa mipira ya juu
    Dk 61, Kichuya anaonekana kupoteza mipira mitatu ndani ya dakika moja. Nakuwa ni kama mtu aliyechachawa hivi
    Dk 60, Gadel anafanya kosa hapa mpira unapitiwa, anapewa Mavugo lakini anaukosa mpira hapa
    SUB Dk 57, Azam wanamuingiza Frank Domayo kuchukua nafasi ya Joseph mahundi


    Dk 55, Simba wanaingia vizuri lakini Muzamiru mpira unamzidi kasi hapa 
    Dk 53, Sure Boy anampiga ngumi Kotei, tena kwa makusudi kabisa, lakini mwamuzi anaonyesha hajaona. Alikuwa karibu kabisa, sasa yuko chini na wachezaji wa Simba wanalalamika
    KADI Dk 50, Banda analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Himid aliyekuwa anakwenda langoni kwao




    Dk 50, Azam FC wanajibu, shambulizi hapa, krosi ya Sure Boy lakini inakosa mtu
    Dk 49, krosi nyingine ya Bukungu hapaaaa, Kichuya anapiga kichwa lakini umbo linakuwa tatizo kwake
    Dk 48, krosi safi ya Bukungu inapita katikati ya lango la Azam
    Dk 47, Simba wanaonekana kufanya masihara hapa, mpira unamfikia Yahya hapa, lakini Mwanjale anajitokeza na kuokoa
    Dk 45 Kipindi cha pili kimeanza na Azam FC wanakuwa wa kwanza kufika langoni mwa Simba, Agyei anajitokeza na kudaka vizuri kabisa

    MAPUMZIKO
    Dk 45+2 Yahya anaachia shuti hapa, lakini Agyei anadaka vizuri kabisa
    KADI Dk 45+1 Himid analambwa kadi ya njano kwa kumkanyaga Bukungu tumboni 

    DKAIKA 3 ZA NYONGEZA

    Dk 44, Agyei anapotea maboya krosi safi ya Sure Boy, Bocco anapiga kichwa lakini mpira unatoka nje kidogooooo
    Dk 43, Manula yuko chini, anadai ana maumivu. lakini inaonekana wazi anachotaka ni kutuliza kasi ya Simba
    SUB Dk 42, Simba wanamtoa Kazimoto na nafasi yake inachukuliwa na Laudit Mavugo raia wa Burundi
    Dk 40, krosi safi ya kazimoto, Manula anapangua na mpira unamkuta Kichuya katika nafasi nzuri lakini anashindwa kufunga
    Dk 36 sasa, mpira unachezwa zaidi katikati ingawa Simba wanaonekana na presha ya kutaka kusawazisha hilo bao


    KADI Dk 33, Sure Boy analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Kotei lakini anamlaumu mwamuzi kwa kupuliza filimbi
    Dk 32, Simba wanagongeana vizuri hapa na Kichuya anaachia shuti kali lakini hajalenga lango
    Dk 30, Simba wanaonekana kucheza zaidi na kusukuma mashambulizi mengi kwenye lango la Azam FC
    Dk 28, Banda anaachia shuti kali la mkwaju wa adhabu lakini Manula anaonyesha umahiri wa juu anapangua na kuwa kona, inachongwa na wachezaji Azam FC wanaokoa
    Dk 26, Krosi nyingine ya Zimbwe, Yakubu anaruka na kupiga kichwa, konaaa, inachongwa na Kotei lakini Azam wanaokoa.




    Dk 25, Simba wanagongeana vizuri na Bukungu anatumbukiza krosi safi hapa lakini Mohammed anaokoa vizuri kabisa
    Dk 21 sasa, kidogo unaonekana kama Azam FC wanapunguza kasi ya mchezo huku Simba wakifanya kila linalowezekana kutaka kupata bao
    Dk 19, Kotei anachia fataki maridadi hapa, lakini mpira unapita juu ya lango la Azam
    Dk 18, Simba wanafanya shambulizi tena lakini krosi ya Bukungu inaishia mikononi mwa Manula
    Dk 15, Azam FC wanafanya shambulizi jingine, Bocco anaachia fataki lakini hakulenga lango

    GOOOOOOOOO Dk 13, Azam FC wanaandika bao safi kabisa, Himid Mao anaachia fataki hapa linalomshinda Agyei na kujaa nyavu za juu
    Dk 10, Azam FC wanafika kwenye lango la Simba, lakini Yahaya anaachia shuti kuuubwaaaaa
    Dk 9, Simba wanaingia vizuri, Kotei anazuiwa na Mkude anaachia shuti kuuubwa juu




    Dk 5 sasa, mpira unaonekana kutokuwa na kasi sana, huenda ni uoga kutoka kwa kila timu kuhofia kuruhu bao la mapema
    Dk 2, Kichuya anatimua mbio kutoka katikati ya uwanja lakini Azam FC wanakuwa makini na kuondosha hatari ndani ya 18
    Dk 1 mechi imeanza taratibu huku kila timu ikionekana kujipanga vizuri tena kwa umakini mkubwa






    SOURCE: SALEH JEMBE.COM

    SOURCE: SALEHJEMBE.BLOGSPOT.COM
    Ili ujue kinachoendelea Mtu wangu usiache kukaa karibu yangu kwenye   FACEBOOK na  INSTAGRAM  @seynation ili niwe nakutumia kila kinachoonifikia.


    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI