Baada ya Young Killer kuachia ngoma yake mpya Sinaga
swaga ambayo ina mistari yenye utata mwingi. leo kwenye
XXL ya clouds fm aliombwa kutolea ufafanuzi moja ya
mstari uliopo kwenye wimbo huo
Sasa baada ya kuwachana/diss baadhi ya wasanii wenzake
Rapper huyo aliamua kumaliza na mstari unaosema "atakae
nijibu ni demu wangu na mkiniacha mnaniogopa" ambao ndio
ameutolea majibu haya
"Sihitaji mjadala uje kuendelea nataka uishie hapa, yani
nimeufunga kisaikolojia" alisema @youngkillermsodokii
Rapper huyo pia ameeleza neno #sinagaswaga kwake
inamaana gani na kudai kwamba mtu ambae hana
swaga ni mtu ambae hana mambo mengi hana mbwembwe,
ni mtu ambae yupo straight
Ili ujue kinachoendelea Mtu wangu usiache kukaa karibu yangu kwenye FACEBOOK na INSTAGRAM @seynation ili niwe nakutumia kila kinachoonifikia.
No comments:
Post a Comment