• Seynation Updates

    Wednesday, 19 April 2017

    BARAKA DA PRINCE HAJANIBANA KIMUZIKI- Naj






    Mwanamuziki wa bongo fleva ambaye pia ni mpenzi wa Baraka The Prince, Naj amekanusha kukatazwa kufanya kazi za muziki na mpenzi wake huyo ambaye naye ni mwanamuziki na kudai usimamizi wa biashara za familia ndiyo unaomuweka kuwa 'busy'
    Naj ameyasema hayo hivi karibuni baada ya kuulizwa juu ya ukimya wake kwenye sanaa na kama mapenzi ndiyo yanayomnyima kufanya kazi zake.
    "Watu hawajui, its not him, mimi mara nyingi kwenye muziki wangu huwa naachaga gap na ni kwa sababu huwa si-focus na muziki pia kama kwa sasa nimeingia mkataba na kina JB wa ku-shoot tamthilia, season 1 tayari kwa sasa tunaendelea na season 2 lakini kitu kingine ni family business ambazo mimi nikiwa huku ndiyo mtu ninayezisimamia nikiondoka ndipo ninapata muda wa kufanya muziki na mambo mengine mengi" alisema Naj
    Kwa upande mwingine Naj amesisitiza kuwa Baraka ndiye mtu ambaye anamsisitiza sana kufanya ngoma na katika wimbo mpya anaotarajia kuachia siku za karibuni mpenzi wake huyo anamchango mkubwa.

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI