Mchungaji Lusekelo amesema hayo alipokuwa akiongea na mtangazaji wa kipindi cha UJENZI kinachorushwa na ting'a namba moja kwa vijana EATV kila Jumapili, Mzee wa Upako anasema mtu anapokufa akiwa ameacha mali za kutosha ni jambo jema kwani familia yake nyuma haiwezi kupata taabu wala watoto hawawezi kupata shida tofauti na yule anayekufa akiwa na kitanda tu kwani watoto wake watapata shida na mateso.
wanamsifia mtu amekufa bila mali alikuwa mwadilifu
"Watu wanamsifu mtu amekufa bila mali eti alikuwa mwadilifu yaani unakuta mtu amefanya kazi serikalini miaka na miaka, sijui miaka 35 au 40 anakufa hata kitanda hana, wapo watu wanasema huyu jamaa alikuwa mzalendo na muadilifu sana hata kitanda hana, hamna mtu huyo alikuwa fala umenielewa huyu alikuwa fala na hastaili kuwa kielelezo cha msingi tuhoji mtu kapata mali wapi? Ndiyo jambo la msingi sababu unaacha watoto duniani unadhani wataishi vipi? Mama anakuwa na nyumba pale anachota kodi anapeleka watoto shule maisha yanaendelea" alisisitiza Mzee wa Upako.