• Seynation Updates

    Thursday, 29 June 2017

    Cristiano Ronaldo athibitisha rasmi kuwa baba wa watoto mapacha


    Mchezaji bora wa dunia anayechezea timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amethibitisha rasmi kwamba amekuwa baba wa watoto wengine wawili wa kiume ambao ni mapacha.


    Mchezaji, Cristiano Ronaldo (katikati) akiwa na familia yake (kulia) ni mama yake (kushoto) ni kaka yake na wakatikati ni mwanae wa kwanza
    Ronaldo ambaye amekuwa akihusishwa kuhamia Manchester United baada ya kuingia katika tuhuma za ukwepaji kodi nchini Hispania, amethibitisha ujio wa watoto hao mapacha mara baada ya timu yake ya taifa ya Ureno kutolewa katika michuano ya mabara inayoendelea nchini Urusi.
    Kwa ujuio wa watoto hao wawili unamfanya mchezaji huyo kuwa na jumla ya watoto watatu kwakuwa tayari alishakuwa na mtoto mmoja wa kiume mwenye umri wa miaka 7.

    Katika mchezo huo wa nusufainali timu ya taifa ya Chile imetinga hatua ya fainali ya Kombe la Mabara kwa ushindi wa mabao 3-0, yote yakifungwa kwa mikwaju ya penalti baada ya dakika 120 za 0-0.

    Kipa wa timu ya taifa ya Chile,Claudio Bravo 
    Kipa wa timu ya taifa ya Chile na klabu ya Man City, Claudio Bravo ndiye ameibuka shujaa baada ya kupangua penati tatu huku Ronaldo akiwa anasubiri kupiga yake “baadaye”

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI