• Seynation Updates

    Friday, 30 June 2017

    DIAMOND KARANGA HAZITAMUACHA MTU SALAMA... SIO ZA MCHEZO MCHEZO


    Diamond Akizindua karanga zake.


    Msanii wa muziki Diamond Platnum amezindua biashara yake mpya ya karanga ‘Diamond Karamba’ zitazokuwa zikipatikana nchi nzima.
    Uzinduzi huo umefanyika Alhamisi hii katika Viwanja vya Karume Jijini Dar es salaam, ambapo muimbaji huyo alizindua bidhaa hiyo huku akidai lengo lake kubwa ni kusaidia kutoa ajira kwa vijana.
    Akizungumza na Bongo5 muda mchache baada ya kuzindua, Diamond amedai yeye ni mfanyabishara kwa hiyo amekuwa akiangalia njia mbalimbali za kufanya biashara ambazo itamwingizia pesa kupitia brand yake pamoja na kuwanufaisha watu wengine.
    “Biashara hii itawanufaisha watu wangi sana, vijana pamoja na wafanyabiashara, tayari mfanyabishara anajua nikilima kwa wingi Karanga soko la uhakika limapatikana. Kwa hiyo hii ni fursa kwa wakulima pia ni njia yangu nyingine ya kujipatia kipato nje ya muziki kwa kutumia brand yangu,” alisema Diamond.
    “Kwa hiyo wanangu wote ambao tunauza Karanga, wataacha kuuza zile zamkononi na kuanza kuuza bidhaa ambayo imefungwa vizuri kwenye mifuko kwa bei nzuri lakini pia mtu ambaye anataka kuzinunua akizuangalia atavutiwa nazo,” aliongeza.
    Hiyo ni biashara ya pili ya muimbaji huyo kwani mapema mwaka huu alizindua perfume ya ‘Chibu Perfume’ ambayo inadaiwa kupatikana nchini nzima.

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI