Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo huenda akafungiwa mechi 05 kufuatia kitendo cha utovu wa nidhamu alichokifanya kwa muamuzi, Ricardo De Burgos katika mchezo wao dhidi ya Barcelona
Ronaldo mwenye umri wa miaka 32, alimsukuma muamuzi, Ricardo De Burgos raia wa Hispania baada ya kupewa kadi nyekundu katika mchezo wa kwanza Supercopa de Espana ambao Madrid ilichomoza na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Barcelona kwenye uwanja wa Camp Nou.
Kutokana na sheria ya soka nchini Hispania kifungu cha 96 kinatumika kwa wachezaji wasio na utovu wa nidhamu kwa kitendo cha kumsukuma muamuzi, kumvuta ama kumtikisa kwa makusudi pindi awapo mchezoni kukabiliwa na adhabu ya kukosa michezo kati ya minne hadi 12.
Tazama video hapa:-