Mdogo wa marehemu Hamadi Ndikumana ambaye alikuwa mume wa muigizaji wa filamu Tanzania Irene Uwoya, anayeitwa Laddy Ndikumana, amesema waigizaji wa filamu wa bongo (bongo movie ) ni wajinga, kutokana na mambo yao wanayoyafanya.
Laddy ameyasema hayo alipokuwa akiongea na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwamba waigizaji hao ni wajinga na wanafiki kwa kuwa wameshindwa kufika kwenye msiba wa kaka yake Ndikumana, ambaye wakati wa uhai wake walijifanya kuwa rafiki yao na kumpenda.
Laddy ameendelea kwa kusema kwamba wakati marehemu Ndikumana alipokuwa na pesa, wasanii hao walikuwa marafiki na kula naye bata, lakini wameshindwa kujitokeza kwenye msiba, na kumuacha Irene Uwoya peke yake kwenda Rwanda.