Manchester United walikosa amani sana baada ya dili la uhamisho wa nyota wa Ufaransa Antoine Griezman ambalo walipambana kwa muda mrefu sana lakini ikashindikana dakika za mwisho.
Baada ya hapo United walimnunua Lukaku lakini ikatajwa kwamba bado wanatega kuhusu Griezman na pia wanaangalia kwa ukaribu maendeleo ya nyota wa Real Madrid Gareth Bale ambaye anaandwamwa na majeruhi.
Lakini sasa yameibuka mengine kwani United wanaonekana wako serious kwenye uhamisho wa nyota kinda wa Real Madrid ambaye siku za karibuni amekuwa gumzo kubwa katika ulimwengu wa soka Marco Asensio.
Habari zaidi zinadai kwamba Asensio na Mourinho wameshawahi kufanya mazungumzo na kama dili hilo likifanikiwa baasi Asensio anaweza kusaini mkataba wa miaka 5 kuitumikia United.
Manchester United wanajipanga kutumka tena kiasi kikubwa zaidi cha pesa katika dirisha kubwa la usajili mwakani na sasa Asensio naye anaingia kwenye rada za Mashetani hao wekundu.