• Seynation Updates

    Thursday 25 January 2018

    Sugu amkataa Hakimu


    Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi "Sugu" na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga, wamemkataa Hakimu Mkazi Mfawidhi Michael Mteite kuendelea kusikiliza yao inayowakabili kwa madai anapendelea upande mmoja na hawezi kutenda haki.

    Kutokana na maombi hayo Hakimu Mkazi Mfawidhi, Michael Mteite ameahirisha kesi hiyo kwa muda wa saa moja ili aweze kutoa hukumu juu ya ombi la washtakiwa kama litakubaliwa au laa.
    Mbunge Sugu aliiambia Mahakama kuwa amejitafakari kwa kina kuhusu mwenendo wa kesi, hivyo anamkataa Hakimu Mteite kuendesha kesi hiyo kwa sababu Hakimu anaegemea upande mmoja kwani walinyimwa dhamana bila sababu za msingi ambazo zipo kwa mujibu wa Kikatiba na Kisheria.
    Sugu alisema sababu ya pili ni kwamba jana alishuhudia kielelezo cha kinasa sauti kikitolewa mikononi mwa Wakili wa Jamhuri na Wakili wa Utetezi alipoomba muongozo alishambuliwa kwa hiyo Hakimu anamaslahi binafsi na kesi hiyo.
    Sababu ya tatu kutoka kwa Mbunge huyo alisema Hakimu alikiri kuwa kesi hiyo inampa shida kuendesha hivyo ili asiendelee kupata shida amemkataa na kuomba wapangiwe Hakimu mwingine wa kuiendesha hiyo kesi. 
    Kwa upande wake Katibu Emmanuel Masonga alisema hana imani na Hakimu huyo kwa sababu wakati wa kuomba dhamana Hakimu alisema anakubaliana na pande zote mbili  kati ya upande wa Mashtaka na Utetezi lakini matokeo yake akazuia dhamana kwa madai ya kuwa kesi iende haraka bila kujali hoja zilizoletwa.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI