• Seynation Updates

    Wednesday 21 February 2018

    DALALI KUMSHUSHA DIAMOND KIMUZIKI NEY WA MITEGO AFUNGUKA MAZITOO.



    Msanii wa muziki Bongo, Nay wa Mitego amefunguka kuhusu kumtabiria Diamond kushuka kimuziki.
    Siku za karibuni Nay wa Mitego alipost picha katika mtandao wa Instagram ikionyesha myama simba akiuawa kikatili, picha hiyo iliamsha hasira kwa mashabiki wa Diamond kwa sababu msanii huyo hutumia jina la simba pia.
    Nay akizungumza na kipindi cha The Playlist cha Times Fm amesema hakukusudia jambo lolote baya kwa Diamond kwa sababu ni rafiki yake na wameshawahi kufanya kazi pamoja.
    “Diamond ni mshikaji wangu, tumefanya kazi kubwa sidhani kama imefikia hatua ya sisi kuwa maadui kiasi hicho na siwezi kumuombea mabaya kiasi hicho lakini tunaona changamoto anazopitia,” amesema Nay.
    “Nilijua tu ile picha wabongo kila mtu ataongea la kwake lakini sina tatizo na Diamond na hata kama lipo basi tutalimaliza ile picha ilikuwa haimuhusu,” amesisitiza.
    Nay amesema sababu ya kuposti picha hiyo ni kupima akili za mashabiki wala kulikuwa hakuna lolote baya. Nay wa Mitego na Diamond wameshafanya kolabo mbili ambazo ni Muziki Gani na Mapenzi Pesa.

    Kwa kutangaza biashara, tukio. au chochote kile kupitia blog hii wasiliana nasi 0684 224 468, 0767 892 902.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI