• Seynation Updates

    Wednesday 4 April 2018

    Mbunge- 'Wimbo wa Taifa SIO rasmi" BASATA kuhusika.


    Katika Kikao cha kwanza mkutano wa 11 wa bunge la Tanzania Mbunge Sixtus Mpunda ameibua mjadala wakati akiomba muongozo kwa Naibu Spika  baada ya kipindi cha Maswali na Majibu. Mbunge huyo amesema kuwa wimbo huo sio ule ulioidhinishwa na BASATA.

    Kwa Mujibu wa Mbunge huyo amesema kuwa wimbo huo una makosa Matatu ambayo ni Ala, Mdundo na Maneno.
    Tokeo la picha la sixtus mapunda

    Pamoja na hayo Naibu Spika Dr.Tulia Ackson amesema kuwa kabla hajatoa muongozo ni lazima ajiridhishe kwanza kwa kuusikiliza, ndipo atakapotoa muongozo'

    Lakini hata kama kutabainika madhaifu kwenye wimbo huo ni hatua gani ambazo zaweza kuchukuliwa? ikiwa ni wimbo ambao wanafunzi pamoja na wananchi wameshauzoea yaani umekuwa Tamaduni, sidhani kama kuna haja ya kubadili chochote kwenye wimbo huu. Yaani ni vema mbunge huyo angeibua hoja ya namna gani ya kuinua sanaa ya Tanzania.
    Wewe Kama Mdau Je? Una maoni gani kuhusu swala hili, tukutane Instagram @seynation 

    Kwa kupata Habari #ChapChap hakikisha ume DOWNLOAD APP yetu kwa KUBOFYA HAPA

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI