• Seynation Updates

    Friday 27 April 2018

    BUNGE YAIKOSOA SERIKALI KUHUSIANA NA SWALA LA KUFUNGIA NYIMBO ZA WASANII.

    Tokeo la picha la banned images


    Kamati ya Bunge ya Huduma za Maendeleo ya Jamii imeikosoa serikali juu ya taratibu zinaotumika na Serikali  kufungia nyimbo za wasanii wa Bongo fleva nchini.

    Kamati hiyo imeeleza licha ya serikali kufungia nyimbo zisizoendana na maadili ya kitanzania hata hivyo kitendo hicho kinaleta changamoto kwa wasanii.
    Akiwasilisha maoni ya kamati hiyo kuhusu bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mwaka 2018/19 kwa niaba ya Mwenyekiti wake Peter Serukamba, mbunge wa Ludewa, Deogratius Ngalawa amesema vyombo vinavyohusika na usimamizi vinapaswa kuhakikisha vinatimiza majukumu yake kwa kukagua nyimbo zote za wasanii kabla hazijatoka.
    “Lengo ni kuhakikisha hakuna wimbo unaotoka kama haujazingatia maadili. Kuangalia nyimbo ambazo ni za kimataifa na kuzipa kibali maalum kwa maana ya muda na mahali pa kuutumia wimbo huo kabla haujaanza kutumiwa na vyombo vya habari,” amesema.
    February 28 mwaka huu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilipokea list ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kutoka kwa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) na kuamuru kutopigwa katika vyombo vya habari. Miongoni mwa wasanii waliofungiwa ni Diamond, Roma, Gigy Money, Snura, Nay wa Mitego na wengineo.
    Usikose habari zaidi Tufuatilie Instagram @seynation na INSTALL APP YETU BOFYA HAPA




    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI