• Seynation Updates

    Friday, 27 April 2018

    TATHMINI YA JUHUDI ZA RC MAKONDA KWA WAMAMA/WATOTO WALIOTELEKEZWA.

    Picha inayohusiana

    Mkuu wa Mkoa Wa Dar Es Salaam Mh.Paul Makonda ametoa tathmini juu ya programu maalumu aliyoianzisha jijini  Dar Es Salaam ya kuwasaidia wamama na watoto walio telekezwa.

     RC Makonda ameunda Kamati ya Wataalamu 15 wakiwemo Wanasheria, Maafisa Ustawi wa Jamii, Jeshi la Polisi Dawati la jinsia na Asasi za kiraia itakayofanya kazi ya kupitia mapungufu ya kisheria na Changamoto zilizojitokeza kisha kutoa mapendekezo kwaajili ya kufikishwa kwa mamlaka husika kwaajili ya maboresho ambapo kamati hiyo itaanza kazi May 05 chini ya Mwenyekiti wake Wakili Albert Msando.
    Aidha RC Makonda amesema tayari amekabidhi Jeshi la Polisi majina ya kinababa waliokaidi wito wake ambapo kwa wale walioko Mikoani barua zitapelekwa kwa Wakuu wa Mikoa na waliopo Nje ya Nchi majina yatafikishwa kwenye Ofisi za Ubalozi kwaajili ya utekelezaji.
    Hata hivyo RC Makonda amesema kupitia zoezi hilo limefanikisha watoto wawili wenye asili ya China kupata matunzo hadi watakapokuwa wakubwa chini ya jumuiya ya Watu wa China.
    Pamoja na hayo RC Makonda amewashukuru wanasheria, maafisa ustawi wa jamii, dawati la jinsia, wataalamu kutoka ofisi ya mkemia mkuu wa serikali na vyombo vya habari kwa kushirikiana nae bega kwa bega kufanikisha Zoezi hilo.
    Usikose habari zaidi Tufuatilie Instagram @seynation na INSTALL APP YETU BOFYA HAPA

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI