Klabu ya soka Yanga imeweka wazi kuwa inatarajia kuondoka nchini wiki ijayo kwenda Algeria tayari kwa mchezo wake wa kwanza katika hatua ya makundi ya Kombe la shirikisho barani Africa dhidi ya USM Alger.
Akiongea leo na wanahabari afisa habari wa Yanga Dismas Ten amesema pamoja na maandalizi ya mchezo dhidi ya Simba April 29, lakini timu hiyo pia inajiandaa na mchezo huo muhimu wa kimataifa.
''Timu inarajia kuondoka nchini Mei 3 kuelekea Algeria ambapo itapitia Dubai na hivyo hivyo baada ya mchezo itarudi kwa kupitia Dubai na maandalizi ya mchezo huo tayari yanaendelea katika kambi yetu mkoani Morogoro'', amesema.
Yanga inatarajia kucheza na USM Alger Mei 6 ikiwa ni mechi yake ya kwanza kati ya sita za makundi ambazo zitachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini na mshindi wa kwanza katika kundi atatinga nusu fainali.
Mabingwa hao wa soka nchini wamefuzu hatua ya makundi kwa kuwatoa Welayta Dicha ya Ethiopia kwa jumla ya ushindi wa mabao 2-1 katika mechi mbili zilizochezwa Dar es salaam na Hawasa huko Ethiopia.
No comments:
Post a Comment