• Seynation Updates

    Saturday 7 April 2018

    ROSE NDAUKA ANAVYOMUENZI KANUMBA.



    Ikiwa leo tar 7/04/2018 ni suku maalum ya kumkumuka marehemu Steven Kanumba , wamejitokeza wasanii katika kumkumbuka Legend huyu.  Rose Ndauka hajabaki nyuma katika kumuenzi shujaa huyu, kwani amefunguka mazito kupitia ukurasa wake wa Instagram. Rose Ndauka ameandika

    Tanzania na Dunia itakukumbuka daima , Ushauri wako bado naufatisha. Waswahili husema Rafiki wa kweli sio yule atakae kupa Samaki ukiwa na njaa Bali ni yule atakae kufundisha kuvua samaki ili kesho uweze kukidhi mahitaji yako hata ukiwa mwenyewe piA uweze kuambukiza ujuzi huo wengine.
    Ulinifunza vyema, nisingekua hapa umekua sababu kubwa ya hapa nilipo. Tutakukumbuka Daima na milele… Rest In Peace Teacher #StevenKanumba #LegendsLiveForever

    Na Pia Ndauka amesema    "Ushauri wako bado naufatisha. Waswahili husema rafiki wa kweli sio yule atakae kupa samaki ukiwa na njaa bali ni yule atakae kufundisha kuvua samaki ili kesho uweze kukidhi mahitaji yako hata ukiwa mwenyewe pia uweze kuambukiza ujuzi huo wengine. Ulinifunza vyema, nisingekua hapa umekua sababu kubwa ya hapa nilipo. Tutakukumbuka Daima na milele... 'Rest In Peace Teacher", amesema Ndauka.

    Marehemu Steven Kanumba alifariki April, 07, 2012, kifo chake kilikuwa cha kushtusha na cha ghafla. Alifariki kwa kuanguka chini alipokuwa kwenye ugomvi wa kawaida na mpenzi wake Elizabeth ‘Lulu’ Michael. Kifo chake kilifichua siri ambayo wengi tulikuwa hatufahamu – kwamba Lulu na Kanumba walikuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI