• Seynation Updates

    Saturday 28 April 2018

    TANZIA: ALIYEKUWA RC DSM, MBEYA ABBAS KANDORO AMEFARIKI



    Aliyekua Mkuu wa mkoa mstaafu Mzee Abbas Kandoro amefariki dunia usiku wa tar 27/04/2018 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini DSM alikolazwa kwa matibabu.
    Kabla ya kifo chake aliwahi kuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Arusha, Singida na Mbeya na mikoa mingine.
    Siku mbili kabla Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alimtembelea na kumpa pole Mkuu huyo wa Mkoa Mstaafu, Abbas Kandoro ambapo awali alikuwa amelazwa katika hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma kabla ya kuhamishiwa Muhimbili DSM ambapo umauti ndipo ulipomkuta.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI