• Seynation Updates

    Wednesday 2 May 2018

    ALICHOKISEMA LEO RAIS MAGUFULI KWENYE UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI IRINGA.



    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewaomba Watanzania wamuombee asije akabadilika na kuwa na kiburi.

    Akizungumza wilaya Kilolo mkoani Iringa katika uwanja wa Luganga, Leo Mei 2 wakati wa uwekaji wa Jiwe la msingi amesema kuwa wamuombee asije akasahau pia ni wapi alikotoka.
    Niwaombe ndugu zangu mniombee, nisije kusahahu nilikotoka, ili niitumikie Tanzania kwa mafanikio makubwa, hata siku nikitoka duniani nikaenda huko, nikaishi kwa furaha kwa sababu niliwatumikia Watanzania wenzangu kwa upendo na mafanikio mazuri,” amesema Rais Magufuli.
    Nataka kuwahakikishia wananchi wa Kilolo, Iringa na Watanzania kwa ujumla sitawaangusha mimi siku zote nitakuwa mtumishi wenu ninajua kuongoza Kiutumishi. Naomba mniombee nisije nikabadilika nisiwe na kiburi.“
    Usikose habari zaidi Tufuatilie Instagram @seynation na INSTALL APP YETU BOFYA HAPA

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI