• Seynation Updates

    Monday 28 May 2018

    ALIYEOKOA MTOTO GHOROFANI, AKUTANA NA RAIS, APEWA URAIA, AAJIRIWA



    MHAMIAJI kutoka nchi ya Mali ametunukiwa uraia wa Ufaransa baada ya kufanya tendo la kishujaa kwa kumuokoa mtoto mdogo aliyekuwa amening’inia kwenye kibaraza cha ghorofa ya nne katika jengo refu jijini Paris.
    Mamoudou Gassama (22) alipanda jengo hilo refu bila kutumia vifaa vyovyote huku akishangiliwa na watu waliokuwa wamekusanyika nje ya jengo hilo, hadi kufanikisha kumfikia mtoto huyo wa kiume mwenye umri wa miaka minne na kumuokoa.

    Soma Pia 'Spiderman' aliyeishangaza Ufaransa kwa kumuokoa mtoto kutoka kwenye jengo la ghorofa

    Kitendo hicho cha kishujaa kilichofananishwa na ushujaa uliwahi kuoneshwa na ‘Spiderman’, uliteka mitandao ya kijamii huku video yake ikivuta hisia za wengi waliotaka atunukiwe uraia na maisha bora kwa kujitoa kuokoa maisha.
    Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron alimualika kijana huyo Ikulu na kuzungumza naye, kisha akampa cheti maalum cha kutambua ushujaa wake na kuamuru apewe uraia wa Ufaransa baada ya kusikia jinsi alivyohangaika kuingia nchini humo.

    Rais Macron amempatia kazi Mamoudou katika Jeshi la Zima moto la Ufaransa, pia amemtunukia medali ya kipekee ya ushujaa kijana huyo na kuwataka raia wote kuiga mfano wake.



    VIDEO YA TUKIO HILO 


    “Nilipowaona watu wamezunguka wanashangaa, sikuwa na muda wa kufikiria, nilikimbia nikavuka barabara kwenda kumuokoa mtoto,” alimwambia Rais Macron.



    “Nilipanda jengo, namshukuru Mungu, Mungu alinisaidia. Kadiri nilivyozidi kupanda nilipata ujasiri wa kupanda zaidi, ilikuwa hivyo, nilipomfikia mtoto nilibaini kuwa tayari mtoto alikuwa na jeraha kwenye mguu wake,” alisema.

    Kikosi cha zima moto na uokoaji kilipowasili kilibaini kuwa tayari mtoto alikuwa ameshaokolewa na msamalia mwema na Mkurugenzi wa kikosi hicho hakusita kutoa pongezi zake kwa muokoaji huku baba wa mtoto huyo anashikiliwa na anahojiwa na jeshi la polisi kwa kosa la kumuacha mtoto mdogo nyumbani bila muangalizi. Mama wa mtoto huyo ameripotiwa kuwa hakuwa jijini humo.


    CREDIT: GLOBAL PUBLISHERS


    Usikose habari zaidi Tufuatilie Instagram @seynation na INSTALL APP YETU BOFYA HAPA

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI