• Seynation Updates

    Tuesday 22 May 2018

    HARRY KANE APEWA KITAMBAA CHA UNAHODHA ENGLAND KWA KAZI MAALUM RUSSIA


    Mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs, Harry Kane, ametangazwa kuwa Nahodha wa kikosi cha timu ya Taifa ya England kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia huko Urusi mwaka huu.

    Kane ameteuliwa na Kocha Gareth Southgate kuchukua nafasi hiyo baada ya kuonesha mchango mkubwa katika klabu yake msimu huu.

    Southgate amemteua Kane zikiwa zimesalia siku kadhaa kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi mapema mwezi ujao.

    Nahodha wa Liverpool, Jordan Henderson pamoja na kiungo wa Tottenham, Eric Dier waliwahi kuwa manahodha wa kikosi cha England chini ya Southgate lakini awamu hii chaguo limemdondokea Kane.




    Usikose habari zaidi Tufuatilie Instagram @seynation na INSTALL APP YETU BOFYA HAPA

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI