Bi Meghan Markle na Mwanamfalme Harry wamevishana pete na kutangazwa kuwa mume na mke Windsor Castle katika sherehe inayofuatiliwa na mamilioni ya watu kupitia runinga, mtandao na redio.
Wawili hao walifunganishwa katika ndoa mbele ya Malkia na wageni 600 waliokuwemo ndani ya kanisa la St George, katika Windsor Castle.
Bi Markle alikuwa amevalia vazi la harusi lililoshonwa na fundi mbunifu wa mitindo Mwingereza Clare Waight Keller.
Bi Meghan alitumia gari aina ya Rolls Royce Phantom kufika kanisani ambapo alipokelewa kwa shangwe na nderemo aliposhuka kutoka kwenye gari hilo na kuingia kanisa la St George.
Miongoni mwa wageni waliofika ni nyota wa televisheni Marekani Oprah Winfrey na mwigizaji Idris Elba.
George na Amal Clooney, David na Victoria Beckham pamoja na Elton John pia wamewasili.
Mwanamfalme Harry na Meghan Markle baadaye walipitia kwenye mji wa Windsor kwa msafara kwa kutumia kigari maalum cha kuvutwa na farasi.
Mwanamfalme Harry amepewa cheo cha Mtawala wa Sussex na bibi yake Malkia Elizabeth II, naye Bi Markle sasa atakuwa Mke wa Mtawala wa Sussex.
Mwanamfalme Harry, ambaye ni wa sita kwenye orodha ya warithi wa ufalme, pia amepokezwa vyeo vya Earl wa Dumbarton na Baron Kilkeel.
Meghan na Harry wakitangazwa kuwa mume na mke |
Mwanamfalme Harry na Meghan Markle katika kanisa la St George, Windsor Castle |
Mwanamfalme Charles (babake Prince Harry) akimsindikiza Bi Markle kumpeleka kwenye madhabahu |
Maelfu ya watu wamefika Windsor kufuatilia harusi hiyo, wengi walikesha kuhakikisha wanapata nafasi nzuri ya kujionea yaliyokuwa yanajiri.
Mwanamfalme Charles, babake Mwanamfalme Harry, ndiye aliyeyemsindikiza Bi Markel kwenda kwenye madhabahu baada ya babake Thomas kushindwa kuhudhuria harusi hiyo kutokana na sababu za kiafya.
No comments:
Post a Comment