• Seynation Updates

    Friday, 1 June 2018

    HIMID MAO KUCHEZEA TIMU YA PETROJET NCHINI EGYPT



    Baada ya siku moja tu tangu klabu ya Azam FC itangaze kumwacha huru nahodha wake Himid Mao, kiungo huyo ameripotiwa kukamilisha kiporo cha usajili wake ambao ulikwama kwenye dirisha kubwa la Juni 2017 katika klabu ya Petrojet ya Misri.
    Akiongea na East Africa Television mapema jana, Himid Mao alithibitisha kuwa anatarajia kuondoka nchini jana jioni kuelekea Afrika Kusini na kisha kuunganisha nchini Misri huku akisisitiza anakwenda kwaajili ya mapumziko lakini ripoti zimeeleza ameshafika Misri na kusaini Petrojet.
    Mao ameelezwa kukamilisha uhamisho wake huo kwa kusaini miaka mitatu ya kuichezea timu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Misri. Msimu wa 2017/18 Petrojet imemaliza katika nafasi ya 12 ikiwa na alama 38 kwenye mechi 34.
    Himid akiwa mwanafunzi wa sekondari alianza kuitumikia  timu ya vijana ya Azam FC mwaka 2011, kabla ya kupata nafasi katika timu kubwa na hatimaye kuaminika zaidi akipata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha Azam FC na timu ya taifa Taifa Stars.
    Kwa upande wa Uongozi wa Azam FC, umeweka wazi kuwa Himid amefuata taratibu zote za kuondoka klabuni hapo na wao kama timu iiyomlea wamemtakia kila la kheri kwenye soka lake nje ya nchi.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI