• Seynation Updates

    Friday, 1 June 2018

    Mfahamu Papa Potwe, kivutio cha utalii kisiwani Mafia Tanzania

    Papa Potwe ni kivutio kikubwa kisiwani Mafia Tanzania

    Je unamjua Papa Potwe? (Whale Shark) ni Samaki mkubwa duniani na huweza kufikia hadi mita 18. Akiwa mdogo huwa na kimo cha basi dogo la abiria.
    Samaki hawa hupatikana maeneo machache duniani, na kwa mujibu wa watafiti wa bahari ni miongoni mwa viumbe vilivyopo hatarini kutoweka.
    Moja ya maeneo wanayopatikana ni kisiwani Mafia Tanzania, sehemu nyingine ni kama Mexico na Philipenes.
    Kutokana na umuhimu wa samaki huyu wavuvi pamoja na wahifadhi wa bahari wamekua na jitihada za kuwalinda viumbe hawa.
    Katika maeneo ya ufukwe wa Mafia mjini, naambiwa kuwa samaki hawa wakubwa duniani ikifika msimu wake basi huonekana hata ukiwa ufukweni, huna haja ya kuingia baharini labda tu ukitaka kuogelea nao.
    Mvuvi akianika Dagaa
    Image captionMvuvi akianika Dagaa
    Papa Potwe hujulikana pia kama Papa mwema kwa ukarimu wake, hufuata wavuvi na watalii wakiwa ndani ya maji na hucheza nao.
    Kwa kipindi cha mwaka mmoja Papa Potwe huweza kusafiri hadi kilomita 10,000.Lakini watafiti wanasema kuwa Papa Potwe wa kisiwani mafia hubaki eneo moja kwa muda mrefu. Katika makala ya National Geographic mtafiti kutoka Marekani, Simon Pierce anasema kuwa hawaendi mbali na inakua kama wanawatembelea rafiki zao wa zamani.
    ''hakuna sehemu nyingi ambapo unaweza kuwaona Papa Potwe wale wale kila mara, na inakua kama utamtembelea rafiki yako wa zamani'' anasema Simon
    Bango linalomtambulisha Papa Potwe
    Image captionBango linalomtambulisha Papa Potwe
    Humphrey Mahudi ni afisa utalii katika hifadhi ya Bahari Mafia, anasema kuwa wamekua wakishirikiana na wavuvi kuhakikisha wanawalinda samaki hawa.
    ''tumekua tunafanya kazi na wavuvi pamoja na halmashauri na wadau wengine kuhakikisha tunawapa mafunzo ya kuwalinda Papa hawa ambao wamo hatarini kutoweka''.
    Kwa upande wa wavuvi wao wenyewe wametengeneza vikundi vya ulinzi shirikishi na jukumu la kwanza ni kuwalinda samaki hawa adimu, kutokana na asili ya samaki hawa hutembea na makundi ya samaki wengi wadogo hivyo ni fursa kwa wavuvi.
    Wavuvi niliozungumza nao wanasema kuwa samaki huyu, kwao hana msimu wanamuona kila siku .
    ramani
    Said Isaa Kombo ni mwenyekiti wa ulinzi shirikishi kwa rasilimali za bahari na ni mvuvi, anasema kuwa mara nyingi hukutana na samaki huyu wakati mwingine wanalazimika kuachia samaki waliwavua ili tuu wampishe wala wasimdhuru samaki huyu.
    ''kama akivuta nyavu zetu na asiweze kujitoa basi tunalazimika kuwasamehe wale samaki wote tuliowavua na kumuacha aende''
    Mbali na jitihada zinazofanyika lakini bado Samaki hawa wanakumbwa na hatari kubwa kutokana na shughuli za uvuvi., na kama jitihada za ziada zisipofanyika basi itabaki historia kuwa kulikuwa na Samaki wakubwa duniani.
    Credit: BBC SWAHILI
    Usikose habari zaidi Tufuatilie Instagram @seynation na INSTALL APP YETU BOFYA HAPA

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI