Golikipa wa zamani wa Real Madrid Francisco Buyo, amejitokeza na kumkosoa nyota wa Barcelona na Argentina Lionel Messi, kuwa hana kiwango kikubwa kama dunia inavyodhani, bali amezungukwa na wachezaji bora ndani ya Barcelona.
''Messi ni mchezaji muongo kuwahi kutokea duniani, anapata mafanikio kwa mgongo wa wenzake na dunia inajua ni yeye'', amesema Buyo kwenye mahojiano na kipindi kimoja na michezo huko Hispania (El Chiringuito).
Buyo ameongeza kuwa Messi angekuwa na uwezo angesaidia timu zake (Barcelona na Argentina) kushinda mataji makubwa kama Ligi ya Mabingwa, Kombe la Dunia na Copa America sio La Liga na Copa del Rey.
Messi msimu wa 2017/18 amefanikiwa kufunga mabao 45 katika michuano yote na kuibuka kinara wa mabao barani Ulaya. Kwasasa yupo nchini Argentina akijiandaa na Fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi kuanzia Juni 14.
No comments:
Post a Comment