Mwimbaji staa wa single ya ‘Amarulah‘ Roberto kutoka Zambia ameshawasili Dar es salaam kwa ajili ya kufanya show Escape one Mikocheni Dsm Dec 11 2015 na kisha Dodoma ambapo kwenye mahojiano yake pia amezungumzia jinsi alivyo na furaha ya kufanya show Dar es salaam kwa mara ya kwanza huku mara yake ya kwanza Tanzania ikiwa ni show aliyoifanya Mwanza.
Kwa upande wa headlines za Dr. Magufuli, Roberto amesema hata Zambia zimewafikia na vyombo vya habari vimekua vikimfatilia ambapo hata Rais wa Zambia amefanya mabadiliko kwenye serikali yake na media zimekua zikiripoti kwamba amefanya hivyo baada ya kujifunza alichofanya Magufuli...
No comments:
Post a Comment