• Seynation Updates

    Friday, 11 December 2015

    Watu waliouawa kwenye machafuko nchini Burundi
    Milio ya risasi na milipuko imesikika usiku kucha katika maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Burundi, Bujumbura.
    Mshauri wa rais Pierre Nkurunziza, ameiambia BBC, kuwa wapinzani wa serikali walijaribu kushambulia kambi kadhaa za kijeshi, katika juhudi za kutaka kuwafungulia wafungwa wanaozuiliwa katika kambi hizo.
    Hata hivyo Nyamitwe, amesema kuwa juhudi hizo za waasi ziligonga mwamba baada ya maafisa wa ulinzi kufanikiwa kuwatimua.
    Ripoti ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa watu kadhaa huenda waliuawa wakati wa makabiliano hayo ya risasi.
    Jeshi la nchi hiyo limefanya msako mkali baada ya matukio hayo na kunasa silaha kadhaa kutoka kwa raia.
    Image copyrightBurundi Police
    Image captionSilaha zilizonaswa na jeshi Bujumbura
    Aidha raia wengi wanasemekana kusalia katika makaazi yao, huku barabara nyingi za mji mkuu, zikiwa hazina shughuli nyingi kama kawaida.
    Ghasia za machafuko zilianza nchini Burundi wakati rais wa nchi hiyo alipotangaza kuwa atawania muhula wa tatu kama rais.
    Zaidi ya watu mia mbili wameuawa tangu machafuko hayo kuanza Aprili mwaka huu.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI