Mtoto wa msanii wa filamu Bongo, Kajala Masanja, Paula Paul anadaiwa kuwa mlevi wa kuogelea ambapo kila wikiendi amekuwa akimlazimisha mama yake ampeleke bichi.
Mtu wa karibu wa Kajala aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini aliliambia Ijumaa kuwa, Paula amekuwa akimsumbua mama yake ampeleke bichi kila ifikapo mwisho wa wiki.
“Yaani yule mtoto ni mlevi wa kuogelea, kila wikiendi lazima akajiache akiwa na marafiki zake na mama yake pembeni,” alisema sosi huyo.
Akizungumzia tabia hiyo ya mwanaye, Kajala alisema: “Ni kweli Paula ni mlevi wa kwenda bichi na sioni tatizo katika hilo. Kwa usalama wake nimekuwa nikienda naye mara nyingi.”
Hivi karibuni Paula alinaswa akiwa sambamba na mama yake katika Ufukwe wa White Sands, Mbezi jijini Dar akila bata, hali iliyowafanya watu waliokuwa ufukweni hapo kumkodolea macho binti huyo kutokana na kivazi alichokuwa amevaa huku akionekana kuchukua figa matata ya mama yake.
Sunday, 27 December 2015
Home
Unlabelled
Kajala: Mwanangu Paula ni Mlevi wa Kuogelea
No comments:
Post a Comment