Mbunge mmoja nchini Kuwait amefariki katika kikao cha bunge.
Video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii imeonyesha mbunge huyo bwana Nabil al-Fadl aliye na umri wa miaka 65 akianguka kwa ghafla kutoka kwenye kiti chake.
Wabunge walimzingira, kisha waziri wa afya (Dr Ali al-Obaidi) akijaribu kumtibu hadi wakati madaktari walipowasili.
Marehemu bwana Al-Fadl -- ambaye alikuwa ni mwandishi wa habari alikuwa maarufu kwa kutumia jarida lake kuwaasa wabunge wenza na hata wakati mwengine kuwakashifu.
Aidha Al-Fadl alifahamika zaidi kwa kuwakaripia waasi wa kiislamu ambao aliwashambulia kwa maneno makali .
Wakati mmoja aliwashangaza wasomaji wake alipoitaka serikali iondoe mara moja marufuku ya uuzaji wa pombe na maeneo ya burudani.
No comments:
Post a Comment