Katika ufunguzi wa mafunzo yayohusu maadili ya viongozi wa umma kwa wakurugenzi watendaji wa halmashauri za wilaya, miji, manispaa na majiji Ikulu Dar es Salaam jana, Kairuki alisema tangu oparesheni ya kutafuta watumishi hewa ianze hadi sasa watumishi 12,246 wamekwishaondolewa.
Kairuki alisema tatizo la watumishi hewa nchini bado ni kubwa na uzoefu unaonesha kuwa nchi nyingi zilizokumbwa na tatizo hilo, huwa naasilimia chache ya watendaji wake ambao ilikua inawajibika na mpaka imeilazimu Serikali kusimamisha masuala mengi ya utumishi wa umma ili ipate taarifa kamili ya aina ya watumishi waliopo, na kwamba wakurugenzi hao wanapaswa kuhakikisha wanasimamia vyema oparesheni hiyo kwani hadi sasa watumishi hewa waliobainika, takribani asilimia 90 wanatokea katika Serikali za Mitaa zinaongozwa na wao kwa sasa.
Licha ya tatizo la Watumishi hewa kumebainika kuwepo na tatizo lingine na utoro wa watumishi wengi sana Serikalini na vile vile akasema endapo Serikali itabaini kuwa maofisa utumishi hao wamehusika kwa namna moja au nyingine katika matatizo hayo ya watumishi hewa na utoro, wataondolewa mara moja.
No comments:
Post a Comment