Kama ulikuwa hujui Linex alitakiwa kuwepo kwenye wimbo ‘Mapenzi’ wa staa wa muziki wa Kenya, Bahati. Lakini akaondolewa kwa madai alizingua
Linex amesema kuna mambo yakitokea kati yake na Bahati ndio maana msanii huyo wa Kenya akafuta verse zake.
“Yeah kweli nilitakuwa kuwepo lakini Bahati alitoa sehemu iliyoimba,” alisema Linex. “Unajua muziki ni biashara, mimi na Bahati tulipanga kushoot video nchini Kenya kwa hiyo nilitakiwa kusafiri kwenda Kenya na nauli nilikuwa ajigharamia mwenyewe na tayari nilikuwa nimeshafanya maandalizi, sasa ile siku napanga kuondoka uongozi wangu kunavitu haukuweka sawa, ikabidi nichelewe kwenda, na kesho yake tulikuwa tunashoot video, kwa hiyo jamaa akaamua kuniondoa kwenye wimbo ndio maana mimi sipo,”
Bahati alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA kuwa walikubaliana na Linex na alisha rekodi sehemu yake na kwamba kilichobaki kilikuwa ni ku’shoot’ video ili kazi hiyo ikamilike, lakini Linex alikuja kumzingua na kumtosa mwishoni, na kusababisha amtoe kwenye wimbo huo, ambao wengi walikuwa hawajui kuwa alishirikishwa Linex.
“Linex sijui ni msanii wa aina gani, tumepanga video kila kitu nimeboook hadi hoteli, akazingua last minute, unajua muziki at the same time tunafunguliana milango, na mimi nilikuwa nataka hii nyimbo iwe ya Linex kuingia Kenya, kwa hiyo alikuja Kenya nikampa verse akaenda poa, tukapanga video, alianza kunipa excuse kwamba meneja hajabook, na yeye ndiye aliyekuwa akiniambia tupange shoot, unajua mi sasa hivi nimewin three times top male artist, sa hii ingekuwa kwa ajili ya yeye kuingia Kenya”,alisema Bahati.
No comments:
Post a Comment