• Seynation Updates

    Saturday, 20 May 2017

    Sasa kimeeleweka Msimbazi: Malalamiko ya Simba kuhusu pointi 3 yametua FIFA.

    Makamu wa Rais wa klabu ya Simba Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amesema, tayari wametuma malalamiko yao FIFA kuhusu pointi tatu walizonyang’anywa na TFF baada ya Kagera Sugar kumtumia mchezaji Mohamed Fakhi aliyekuwa na kadi tatu za njano walipocheza dhidi mechi ya ligi dhidi ya timu hiyo ya Bukoba.
    Kaburu amesema barua yao ya malalamiko imepokelewa na FIFA na wanachosubiri ni kusikia uamuzi gani utatolewa na shirikisho hilo la soka Duniani.
    “Tumeshatuma malalamiko yetu na yamepokelewa FIFA, tumeainisha tunataka nini. Nisiwasemee, wao watasoma na wataamua halafu watatujulisha walichokiamua,” amesema Kaburu wakati akizungumza na Clouds FM kupitia kipindi cha michezo Sports Extra.
    Simba walifikia uamuzi wa kupeleka jambo hilo FIFA baada ya Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi za wachezaji kutengua uamuzi wa Kamati ya saa 72 ambayo awali iliipa Simba pointi tatu na magoli matatu baada ya kubaini ni kweli Kagera Sugar ilimchezesha Fakhi dhidi ya Simba huku akiwa na kadi tatu za njano kinyume na kanuni.
    Kwa sasa Simba ina pointi 65 ponti tatu nyuma ya Yanga huku timu zote zikiwa zimesaliwa na mechi moja ili kuhitimisha ligi msimu huu.
    Kama FIFA itaamuru Simba ipewe pointi tatu wanazozilalamikia zinaweza kuwasaidia kunyakua ubingwa wa VPL ikiwa Yanga watafungwa au kutoka sare kwenye mchezo wao wa mwisho dhidi ya Mbao halafu Simba ipate ushindi kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Mwadui FC.

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI