Usaili wa viongozi wanaowania nafasi ya uongozi katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), unaendelea.
Mchujo huo wa viongozi unafanyika katika Ofisi za TFF, Karume jijini Dar es Salaam huku wagombea wawili, Jamal Malinzi aliyekuwa akiwania urais na Geofrey Nyange 'Kaburu' aliyekuwa anawania umakamu Mwenyekiti.
Uchaguzi umepangwa kufanyika Agosti 12 mjini Dodoma na Malinzi ndiye anaishikilia nafasi ya Rais wa TFF..