• Seynation Updates

    Thursday 16 November 2017

    POGBA NI KIUNGO MUHIMU SANA UNITED...MAJERAHA YAKE YAWAGHARIMU LUKAKU NA MHIKITARYAN



    Baada ya mwanzo mzuri katika msimu huu akifunga magoli 11 katika mechi 10 za kwanza, Romelu Lukaku alitegemewa kuendeleza moto wa ufungaji, hata hivyo tangu alipofunga goli lake la 7 katika Premier League mnamo September 30, Lukaku amepatwa na ukame mkubwa, akicheza mechi 7 mfululizo katika mashindano yote bila kufunga goli.
    Wakati suala la ukame ni jambo la kawaida ambalo linawakuta washambuliaji wengi – Robin Van Persoe alicheza mechi 13 chini ya Sir Alex Ferguson bila kufunga – jambo linalompa wakati mgumu Jose Mourinho kuhusu hali ya uchezaji kiujumla ya Lukaku, hasa tangu Paul Pogba alipopata majeruhi.
    Katika mchezo wa mwisho wa Manchester United katika EPL, dhidi ya Chelsea, Lukaku aligusa mpira mara 24 tu. Alishindwa kujihusisha zaidi na mchezo na alikuwa amepotezwa kabisa. Sio ya makosa yake yote, sapoti kutoka kwa viungo wake haikuwa inayojitosheleza, kwa kifupi haukuwa mchezo mzuri kwake.

    Ukiangalia upande wa Bluu Alvaro Morata, aligusa mpira mara 51, hapa utaona mshambuliaji huyu Kibelgiji hakuwa na influence ya kutosha mchezo na hii imekuwa kawaida katika michezo mikubwa yote msimu huu.
    Dhidi ya Liverpool, katika dimba la
    Anfield, Lukaku aligusa mpira mara 22 tu, wakati Robert Firminho aligusa mpira mara 58 katika dakika 87 alizocheza. Tofauti kubwa baina ya washambuliaji hawa wa timu mbili – takwimu zinazotia mashaka kwa Lukaku.
    Mourinho amekuwa akimtetea Lukaku kutokana na kiwango chake, lakini kuna mambo ya kuangalia kwanini kiwango kimeshuka. Hakuna shaka kutokuwepo kwa Pogba kumechangia sana kuporomoka kwa nguvu kwenye mashambulizi kiujumla ya timu.
    Pogba ndio “nuklia” ya timu kwenye kuunganisha safu ya kiungo na ushambuliaji. Hakuna mchezaji kwenye timu ambaye anafikia unyumbulifu na ubunifu wa Pogba na ndio maana kutokuwepo kwake kumeiathiri saba timu.
    Ander Herrera sasa ndio mbadala wake kwenye kiungo, lakini mchezaji huyo wa zamani wa Athletic Bilbao hana uwezo wa Pogba. Hana nguvu, wala ufundi, achilia mbali kimo chake. Kuna vingi vya kuongelea kuhusu mchezaji kiungo na sifa zake, viungo wengi wa kati waliofanikiwa ni wale wenye nguvu na ubunifu.
    Tatizo lingine linaloiagharimu United, ni Henrikh Mikhitaryan. Ingawa amecheza kwenye timu kwa muda wote, kiwango chake kimeporomoka kwa kiasi kikubwa na anastahili kukaa benchi kwa sasa, pamoja na kwamba alianza ligi vizuri akitoa assists 5.
    Wakati Manchester United ilipocheza na Stoke City ugenini katika sare 2-2, alipiga pasi 106, 93 kati ya hizo zilifika. Katika mchezo huo huo Mhikitaryan ambaye alicheza mbele ya Pogba alikamilisha pasi 48.
    Dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Stamford Bridge, Mhiki alikamilisha pasi 19 tu.
    Hilo linakuonyesha wazi namna Pogba alivyo muhimu katika kuunganisha safu ya kiungo na ushambuliaji ya timu na kuzisababishia matatizo timu pinzani.
    Ni kweli kuna utofauti wa ubora kati ya Chelsea ba Stoke, lakini hapa pointi inabaki kwenye ukweli kwamba Pogba anaweza kuumiliki mpira na pindi anapokuwa na mpira kunakuwa na urahidi wa wachezaji wengine kuhuusika zaidi na mchezo na kuleta matatizo kwenye lango la wapinzani. Mkhitaryan anaonekana amekosa muelekeo bila Pogba, jambo ambalo linapelekea Lukaku kukosa usaidizi mbele.
    Lukaku jana ametimiza magoli 31 katika mechi 64 alizoitumikia nchi yake na kuweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa nchi hiyo, lakini kiwango chake akiwa na Uzi mwekundu wa United imekuwa hakiridhishi.
    Kifuatacho ni kipindi cha Christmas, kipindi muhimu ambacho mechi zinakuwa ngumu na nyingi. Habari nzuri kwa United Pogba atakuwa fiti kuanzia mchezo ujao dhid ya Newcastle, wakati atahitaji muda ili kurudi kwenye kasi yake – uwepo wake utaisadia kuirudisha United ambayo ilianza msimu huu kwa soka zuri na linalozalisja magoli mengi.

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI