• Seynation Updates

    Thursday, 16 November 2017

    GIGY MONEY AFUNGUKA KUHUSU UGOMVI WAKE NA MJUMBE........

    Msanii Gigy Money ambaye hivi karibuni amezua gumzo na kushangaza watu baada ya kuona mahali anapoishi, amesema ni kweli sehemu ambayo anaishi kwa sasa hapafanani na yale anayoyafanya, lakini hata hivyo hajutii hilo.
    Akiongea kwenye 5SELEKT ya East Africa Television, Gigy Money amesema nyumba ambayo imeonekana anaishi sasa amehamia hivi karibuni baada ya nyumba aliyokuwa anaishi awali kujaa maji na kusomba vitu vyake, kutokana na mvua zilizoleta mafuriko hivi karibuni.
    Gigy Money ameendelea kwa kusema kwamba kitendo cha mafuriko kusomba vitu vyake kimempa 'stress' kwani imemlazimu kuanza moja kwenye maisha, pamoja na kutafuta nyumba yoyote ile ili aanze maisha upya.
    “Unajua nimetoka kwenye mafuriko, nyumba niliyokuwa naishi mwanzo maji yalijaa yakasomba vitu vyangu vyote, stress niliyonayo mimi mwenyewe ndo najua, yani naanza maisha moja ndio nikatafuta nyumba nikapata hapa, pale ninapokaa hata sistahili kukaa pale ndio naanza moja na mimi binadamu”, amesema Gigy Money.
    Hivi karibuni kumeibuka minong'ono kwa baadhi ya watu wakionesha kushangazwa na kitendo cha Gigy Money kuishi kwenye nyumba ambayo haieleweki wakati mitandaoni anajitapa kuvaa vitu vya gharama kubwa zaidi.

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI