• Seynation Updates

    Monday, 15 January 2018

    NDOA YA WOLPER KUVUNJA REKODI 2018 ITAFANYIKA BONGO NA KWA TRUMP

    Ndoa ya Wolper si ya Nchi Hii....... Kufanyika Bongo na Marekani

    ILE sherehe ya ndoa yaani harusi ya staa mkubwa wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper Massawe itakuwa na mbwembwe ambazo si za nchi hii kwani itafanyika Bongo kisha Marekani.


    Katika mahojiano maalum, Wolper alilieleza Ijumaa Wikienda kuwa, harusi hiyo itafanyika hivi karibuni na inatarajiwa kuwa ya gharama kubwa kwani itaacha historia.

    Wolper alisema kuwa, harusi hiyo itagharimu takriban shilingi milioni 60.

    “Milioni kama 50 zitatumika kwenye sherehe ya hapa Bongo na nyingine 10 nje kwa sababu kule Marekani hatutakuwa na watu wengi sana,” alisema Wolper.

    Wolper alisema kuwa, katika sherehe ya Marekani itabidi aende na wasanii wanne tu wa Bongo ambao atawalipia nauli ya kwenda na kurudi na kuwapa pesa ya kujikimu.

    “Wasanii ambao nitaenda nao kwa ajili ya kuhudhuria harusi yangu ni wanne tu, mmoja kati yao ni Aunt Ezekiel kwa sababu huwa ananipa sapoti kwenye biashara zangu hivyo siwezi kumwacha,” alisema Wolper ambaye hivi karibuni alitolewa mahari .

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI