Halmashauri ya mji wa Mbinga mkoani Ruvuma imewafukuza kazi watumishi wake 58 kwa makosa mbalimbali ikiwemo kughushi vyeti vya kidato cha nne na wengine kwa kuisababishia hasara halmashauri hiyo.
Uamuzi huo umetangazwa na Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Mbinga Mheshimiwa Egno Kipwere ambapo watumishi waliofukuzwa kazi ni wa kada mbalimbali wakiwemo walimu na Maofisa Watendaji pamoja na Afisa Misitu wa halmashauri hiyo Bw. David Hyera.
No comments:
Post a Comment