• Seynation Updates

    Tuesday 24 April 2018

    Binti wa miaka 24 anayetarajia kufunga ndoa na Rais Wa Afrika Kusini Zuma, Tayari Amezaa Naye

    Binti wa Miaka 24 Anayetarajiwa Kuolewa na Zuma Alazimishwa Kujiuzulu

    Mwanamke ambaye anatarajiwa kuwa mke wa saba wa aliyekuwa rais wa Afrika kusini,Jacob Zuma amelazimishwa kujiuzulu ajira yake ya ukuu wa asasi isiyokuwa ya kiserikali na chombo cha habari cha nchini humo, asasi iliyokuwa ikijishighulisha na maswala ya kupinga Mabinti kuolewa na Vizee 
    Nonkanyiso Conco ambaye ana mahusiano ya kimapenzi na bwana Zuma ambaye amemzidi umri wa miaka 52

     Wakati huo yuko kwenye asasi inayohamasisha kampeni ya kuwawezesha mabinti wadogo katika maisha yao ya kila siku na kuacha kuwategemea wanaume wenye umri mkubwa.
    Bi.Conco mwenye miaka 24 amejifungua mtoto wa Zuma katika hospitali ya binafsi iliyoko mjini Durban.
    Zuma kwa sasa ana umri wa miaka 76,ana wake wanne na mwingine mmoja waliachana na mke wa sita alijiua mwaka 200 pamoja na watoto ishirini.

    Conco analazimika kujiuzulu cheo chake akiwa ni afisa mawasiliano wa kampeni ya kukabaliana na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa wanawake wadogo, unyanyasaji wa kijinsia na ujauzito kwa watoto wadogo.Mpaka sasa Bi Conso hajazungumza chochote kuhusiana na tuhuma zinazomkabili lakini amewasilisha barua ya kujiuzulu kazi katika shirika analofanyika kazi,Daily Maverick limeripoti.
    Habari za mahusiano ya Jacob Zuma na Bi Nonkanyiso Conco zilizagaa sana tangu siku ya ijumaa iliyopita .

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI