• Seynation Updates

    Tuesday 24 April 2018

    Tusilolijua Kuhusu ZITO KABWE na Mahala alipo.

    Katibu wa uenezi wa Chama cha ACT WAZALENDO Ado Shaibu ameweka wazi juu ya swala zima la Zitto Kabwe. Ado amesema kuwa Zitto Kabwe hajapotea, wala hajatekwa bali yupo chini ya Uangalizi yaani ameongezewa ulinzi na mienendo yake inachunguzwa.

    Tokeo la picha la ado shaibu
    Ado Shaibu


    Ado amesema kuwa kumekuwa na Taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Zitto Ameuawa na huebda ametekwa, na hio ndio sababu kubwa ya kumuwekea ulinzi wa kutosha Zitto Kabwe.

    "Ukisikia kwamba kiongozi wenu anataka kushambuliwa, kudhuriwa au kuuwawa ni muhimu kuyapa uzito sana maneno hayo kwa hiyo sisi tumechukua hatua kadhaa kwanza ndugu Zitto alikuwa na mkutano wa hadhara Kigoma Ujiji alikuwa anataka kuzungumzia masuala yanayoendelea nchini kuhusu ripoti ya CAG lakini alitaka kuwaeleza watu wa Kigoma wapi amefikia kuhusu suala la watu wa Kigoma kunyanyaswa uhamiaji na kutaka maoni ya wananchi kwa hiyo mkutano wenyewe huo ulizuiwa na sisi tulikuwa na mkutano wa ndani wa chama kutokana na mambo haya yanayoendelea tukaamua ni bora tusimamishe kikao hicho" alisema Shaibu

    Ado Shaibu aliendelea kusema kuwa

    "La pili kiongozi wa chama ameongezewa ulinzi na idara ya ulinzi na usalama ya chama kuhakikisha kwamba anakuwa salama na kuchunga mienendo yake ndiyo maana utaona baadhi ya magazeti yanasema Zitto Kabwe amefichwa, ndugu Zitto ni kiongozi hawezi kufichwa lakini mienendo yake sasa inadhibitiwa na idara ya ulinzi na usalama ya chama awe wapi, muda gani na kwanini, awe ndani ya nchi, nje ya nchi hayo ndiyo mambo ambayo idara yetu ya ulinzi na usalama inayapa kipaumbele kikubwa, kwa hiyo kiongozi sasa analindwa kwa daraja ya juu" alisisitiza Ado Shaibu

    Baada ya Zitto Kabwe kuonekena ameikomalia sana ripoti ya CAG hasa zaidi kuhusu 1.5 Trilioni ambayo haileweki imetumikaje zilianza kusambaa taarifa mbalimbali kuwa kiongozi huyo naye anaweza kushughulikiwa na watu wasiojulikana.


    Usikose habari zaidi Tufuatilie Instagram @seynation na INSTALL APP YETU BOFYA HAPA

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI