• Seynation Updates

    Saturday 14 April 2018

    Goodluck Gobert Alichokisema banda ya kutoka Ikulu. 🙏



    Msanii wa nyimbo za Infill ajulikanae kama Goodluck Gozbert anae fanya vizuri na wimbo wake uitwao hauwezi Kushindana,  aliweza kualikwa ikulu na Mh. John Pombe Magufuli,  hii ni kutokana na kipaji alichokuwa nacho msanii huyu,  hali iliyopelekea Rais kumuita ikulu.
    Gozbert aliandika kama ifuatavyo kwenye Ukurasa wake wa Instagram 👇

    "Nikukumbushe Tu....Sikuzaliwa Kwenye Familia Yenye Kujulikana au Kuwa Na Heshima Kokote Kule,  na Wala Sikuwahi Kushika hata Nafasi Ya Tano Darasani,  Nakumbuka Kuchekwa,  Kukatishwa Tamaa,  Kuandikiwa Ubaya, Kunenewa Uongo Na Kutabiriwa Kushindwa kila Nilipofikiri Ningeweza, Nakumbuka Mengi Mengine Ya Juzi Tu.....!!!! Ila Hakuna kitu nakumbuka Zaidi Kama Zile Ahadi Za Mungu Kwangu, Hakuna Kitu  Nakumbuka Kama Huruma Za Huyu Yesu Aliyenipenda Nikiwa Sijielewi.....!!!! Kesho Nitawaambia Wanangu, Mungu Aliyenitoa na Kunifikisha Pale Ndiye Atakayeenda Pamoja Nanyi.
    #MUNGU NINAKUSHUKURU TENA"- aliandika Gozbert


    Endelea kufuatilia kila kina make headlines kupitia blog hii ya seynation Tukutane mitaa ya Instagram @seynation

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI