• Seynation Updates

    Saturday 14 April 2018

    Msidhani Nandy ana moyo wa chuma.... A-Z kuhusu Nandy X Bilnass na Video Yao

    Msanii Nandy ameshika headlines wiki hii baada ya kusambaa kwa video ya utupu akiwa na msanii mwenzake Bilnass. Kutokana na hilo Mashabiki waliibua mengi na mazito juu ya Nandy ni pamoja na kupata uthibitisho kuwa Nandy na Bilnass ni Wapenzi kwani kulikua na tetesi tu bila uthibitisho.
    Tokeo la picha la NANDY

    Hata hivyo nandy anaonesha kushangazwa na video hio iliyosambaa, jambo ambalo limemkosesha Raha kabisa.Kupitia  ukurasa wake wa Instagram anasema
         " “Kiukweli niko katika wakati mgumu wa maisha yangu.. jana sikuwa sawa ila leo nimeweza hata shika simu yangu najua matusi yote na fedhea kutoka kwa mashabiki wangu ni sababu wanaamini hili ni kusudio letu au langu hii video iwe public naapa na naumia sana sana kwa hili lilitokea!!! sihusiki na kusambaza video wala siwezi ruhusu kitu kama hichi kitokee kwenye maisha yangu ya usanii hata ya kawaida” Aliandika Nandy


    Kupitia U-heard ya Soudybrown Nandy amesema kuwa video hio sio yeye aliyoismbaza na pia video hio ni ya zamani Mwaka 2016 na hajui nani aliyoisambaza, Pia Kupitia Instagram amesema
         " “Sitakiwi kujieleza sana ila naamini nikiandika hili nitakaa na amani kwa ambaye ataamuaa kuendelea kunihukumu aendelee tu kunihukumu kwani kweli nimekosea ila ajiulize kama yeye hajawahi kukosea!” -Nandy

    “Mambo yetu wote ya private yanatakiwa kubaki private, aliyeyatoa amefanikiwa kuleta hii taharuki, sintofahamu na maumivu makubwa ambayo sijawahi kupata maishani mwangu. ila Naamini sababu kuu ya hii video kuwa out ni mambo ya simu zetu ambayo inaweza kumtokea mtu yoyote!!” -Nandy

    “Nilibadili simu yangu mara 2 toka 2016 na Bilnas aliibiiwa simu yake huko nyuma, kwa mujibu wake, so hatujui mpaka sasa imetoka kwa simu ya nani? maswali ni mengi matusi ni mengi simu na sms ni nyingi mnoo… naumiaa naumiaa kupita kiasi.” -Nandy

    Tar 14/04/2018 Nandy alipata nafasi ya kuonana na BASATA, ambapo Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Godfrey Mngereza amesema mwanamuziki Nandy ambaye picha zake za utupu zilivuja anahitaji kupewa moyo kwa kuwa tukio hilo limemuumiza.

    Amesema jamii iache kumlaumu mwanamuziki huyo, kwani kilichompata kinaweza kumtokea yeyote hasa katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia.


    Amesema kama Baraza wamemuita na kuongea naye kwa ajili ya kumpa moyo na kueleza hayupo katika hali nzuri kwa sasa na anahitaji kupatiwa ushauri wa kisaikolojia.


    Wewe ukiwa kama Mdau, Shabiki wa Nandy hebu tukutane instagram @seynation







    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI