• Seynation Updates

    Wednesday 11 April 2018

    Swala la Wanafunzi wenye Ujauzito kutorudi shule lapigiliwa msumari.



     Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha amesema kuwa serikali haitarajii kuwarudisha wanafunzi waliopata ujauzito shuleni kwa njia yoyote ile. Ameyasema hayo katika kikao cha bunge Mjini Dodoma.

    Naibu waziri pia amesema kuwa itakuwa ni uchochezi wa matendo ya ngono mashuleni, endapo wanafunzi wenye ujauzito wataruhusiwa kurejea shuleni.


    “Hata sisi serikali kwa kweli hatupendi kusikia vitendo vya uonevu dhidi ya watoto wa kike kwasasa mfumo wetu wa elimu umepangwa katika namna ya kuhakikisha wanafunzi wanafunzi wanaopata ujauzito wanapata fursa ya kuoa lakini nje ya mfumo rasmi kwahiyo kuna fursa nyingine nyingi za kusoma kama nilivyosema katika swali langu la msingi kupitia elimu ya watu wazima lakini vilevile vyuo vya ufundi,“ amesema Nasha.
    “Serikali haitarajii na naomba niweke wazi wanafunzi ambao wamepata ujauzito kwa njia yoyote ile na kwasababu ukifanya hivyo ndio maana yake una halalisha na kuhamasisha ngono mashuleni wakati mila zetu na sheria zetu haziruhusu ngono katika shule maana yake katika shule za msingi na sekondari.“

    Usikose habari zaidi Tufuatilie Instagram @seynation na INSTALL APP YETU BOFYA HAPA

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI