• Seynation Updates

    Friday, 25 May 2018

    Hesabu Kamili ya Yanga FC Na Azam FC

    Ikiwa ligi kuu soka Tanzania Bara inafungwa rasmi Jumatatu ya Mei 28, 2018, klabu za Yanga SC na Azam FC ambazo zinawania nafasi ya pili zitakipiga usiku kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi.
    Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Shirikisho la soka nchini TFF, michezo yote ya mwisho wa ligi siku ya Jumatatu itachezwa muda mmoja isipokuwa mchezo mmoja wa Yanga na Azam FC ambao utapigwa usiku.
    Mechi 7 ikiwemo ya bingwa mpya Simba dhidi ya Majimaji zitapigwa saa 10:00 Jioni, ambapo mbali na bingwa kupatikana tayari timu moja imeshashuka daraja ambayo ni Njombe Mji.
    Azam FC wakiwa nyumbani Chamazi watakipiga na Yanga kuanzia majira ya saa 2:00 usiku ambapo mshindi wa mechi hiyo ndio atamaliza wa pili kwenye msimamo wa ligi msimu wa 2017/18.
    Mechi zote nane
    Lipuli vs Kagera Sugar- saa 10 kamili
    Tanzania Prisons vs Singida Utd- saa 10 kamili
    Ndanda vs Stand Utd- saa 10 kamili
    Mtibwa Sugar vs Mbeya City- saa 10 kamili
    Yanga vs Azam- saa 2 kamili usiku
    Njombe Mji vs Mwadui- saa 10 kamili
    Mbao vs Ruvu Shooting- saa 10 kamili
    Majimaji vs Simba- saa 10 kamili

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI